Everything below is correct in meaning, and spelling!!
Jifunze Kiingereza: English for Swahili Speaking People.

I like rice: Napenda Mchele.
We have a cat: Tuna paka.
I have a bath everyday: Naoga (nyumbani) kila siku.
Ask the Children to bring me my pipe: Waombe watoto waniletee kiko changu.
Last night I could hear a Lion outside our house: Usiku niliweza kusikia simba nje ya nyumba yetu.
We get our sugar from the Indian shop: Twapata sukari yetu katika duka la kihindi.
The maize is getting ripe: Mihindi inaiva.
Keep a watch on this man I think he s a thief: Mwangalie mtu huyu; nadhani yu mwizi.
I keep my clothes in a box: Naweka nguo zangu katika sanduku.
This is the hen that eats the eggs: Huyu ndiye yule kuku alaye mayai.
I know how to speak English: Najua (jinsi ya) kusema Kiingereza.
I have finished feeding the fowls, what shall I do know? Nimekwisha kuwapa kuku chakula; nifanyeje sasa?
Poisonous trees: Miti yenye sumu.
My field is larger than yours: Shamba langu ni kubwa kuliko lako.
The roots of this tree are more poisonous than the leaves: Mizizi ya mti huu ina sumu kuliko majani.
They say the buffalo is the most dangerous of all wild animals: Husema nyati ndiye mwenye hatari katika wanyama wote wa mwituni.
When we found the man he was nearly dead: Tulipomwona mtu alikuwa karibu na kufa.
Turn the coat inside out: Geuza koti upande wa ndani nje.
I hear the cry of an Owl: Nasikia sauti ya bundi.
When I got to my field I found monkeys there: Nilipofika shambani kwangu nilikuta manyani huko.


© 'Crazy Ad Productions' 2002/2003